Download Swahili
Dibaji
Kitabu hiki ni matokeo ya kazi niliyofanya maishani mwangu, neno la mwisho ambalo ningependa kutoa kuhusu maudhui ambayo nimekuwa niking’ang’ana nayo tangu nilipokuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Khartoum, Sudan, katika miaka ya mwisho ya miaka ya sitini. Katika kitabu hiki mimi nasema kama Mwislamu kwa sababu hii kama dini yangu inanifanya kuwajibika kufanya hivyo, na sio tu kama jambo la kimjadala la kisomi. Lakini, mimi hapa natetea juu ya dola ya kisekula, au dola ambayo hailemei upande wowote wa kidini kama mfumo wa kujadili juu ya mustakabali wa Sharia, bila ya kudai au kutafuata kuangalia kwa undani athari za kinadharia au kitekelezi za nadharia hii. Katika maelezo haya ya mwanzoni, mimi natafuta tu kuanzisha mjadala kuhusu mambo haya, kuliko kutaka kutoa masuluhisho. Kile ambacho huenda kikatokea kutoka kwenye mjadala ambao ninautoa itategemea sana juu ya vile Waislamu wanavyohisia, kupata, kurekebisha au kukataa pendekezo langu. Pia ningependa kusisitiza kwamba yale ambayo napendekeza hapa yanahusiana na kazi ya Sharia hadharani, au maeneo ya kiumma, na sio mambo ya itikadi za kidini na utekelezi katika maeneo ya faraghani ya mtu kibinafsi. Tukianzia na wazo kwamba Sharia haina budi kuchangia kwa kiasi kikubwa katika maisha ya umma katika jamii za kiislamu, mimi ninajishughulisha hasa na kufafanua na kulinda zile hali zinazofaa kabisa kwa kujadili kazi hiyo.
Mambo mengi kati ya yale ambayo mimi napendekeza tayari yamewahi kupendekezwa na wataalamu wa Kiislamu wengine, jambo ambalo ninaliona ni la kutia moyo sana kwa sababu linaonyesha kwamba pendekezo langu linaweza kufaidika kutokana na kulundika kwa mambo ya kutoa manufaa sana na mijadala. Kwa vile mimi ninatilia maanani zaidi uwezo wangu wa kuweza kushawishi, na sio kudai uandishi wa kipekee ambao haujawahi kusambazwa, ninakuta kuwa ni jambo la kufaa na kunihakikishia kwamba mimi si mtu wa pekee ambaye anasema jambo hili. Kma vile n,itakavyojadili katika sehemu mbali mbali za kitabu, dola haijapata kabisa kuwa ni ya kiislamu, ijapokuwa haikuwa ya kisekula kikamilifu kwa maana ambayo ninaipendekeza hapa. Kutokana na hivyo basi, mimi najaribu tu kuchangia katika kule kufafanua kile ambacho tayari kimekuwa kitu halisi katika jamii za kiislamau tangu mwanzoni kabisa kwa kuikuza hali ile ya uhalisi wa kihistoria na kuitia katika mfumo wa kufaa kwa siku za usoni. Kile ambacho natarajia kuchangia ni kuleta pamoja mambo mbali mbali pamoja, hasa ile nyanja ya ukatiba, haki za kibinaadamu na uraia, kwa namna ambazo zinawezesha utekelezi wa kitendaji wa mfumo unaopendekezwa kwa kusimamia uhusiano baina ya Uislamu, dola na jamii.
Kwa madhumuni hayo, nimefikiria na kufanya utafiti ambao unaelezwa katika kitabu hiki kwa namna ambayo inatoa nafasi ya mbele ya kueleza fikira zangu hizi ambazo kwa sasa hazijapevuka ili kujadiliwa katia ya wataalamu wa kiislamu na viongozi wa jamii. Kwa kufanya hivi, nimetafuta kulikabili lile jambo la umuhimu wa kuweko kwa ushawishi katiak kufikiria na kuendeleza nadharia yenyewe, kuliko kule kufanya hivyo tu baada ya kuchapishwa. Tanzu ya mjadala wa hadharani wa utafiti huu ulikuwa ni moja katika sehemu zake za mpango wa mwanzo kwa misingi yake ya kinadharia na matokeo yanayotumainiwa. Kwa upande mmoja, nilijaribu kuendeleza mawazo yangu na athari zake kutokana na faida na tafakuri za mawazo na hivi karibuni kabisa na yale ambayo yamejaribu kutuelekeza kwenye siku za usoni juu ya maudhui haya ambayo huenda yakawa hayapatikani katika namaba ya kuchapishwa. Pia tangu mwanzo nilipanga kuhusisha uchambuzi wangu na sera za umma na utekelezi wa uhalisi tangu mwanzo kabisa wa harakati hii. Na kwa upande mwingine, nilijaribu kutafuta nijia za kuchangia katika mawazo ya sasa, na hapo hapo huku nikipima kufaa kwake na uwezekano wa kufaulu kwa mawazo yangu, pamoja na kufanya bora na kuchonga uwezo wangu wa kuyawasilisha kwa namna ambao itafaulu. Hivi ni kusema kwamba, nilijaribu kukariri kazi yenyewe ya kutetea mabadiliko kulingana na nadharia inayopendekezwa katiaka zile harakati za utafiti na kuandika, kwa kujaribu kutambua yale ambayo huenda yakaleta upinzani na kufikiria majibu ya kufaa dhidi ya upinzani huo badala ya kutoa mawazo ya mwisho kabisa ambayo yametungwa kwenye upweke wa kiakademia. Mimi ninashughulishwa zaidi ya uwezo wangu wa kushawishi kama vile ambavyo nilivyo na kuwepo kwa kudhibitika na kushikana sawa sawa kwa nadharia katika matokeo ya utafiti huu.
Kwa hivyo, nilianza harakati hii kwa kwanza kabisa kuandika “karatasi ya kwanza ya fikira zangu” ambayo ilisambazwa na kujadiliwa na wataalamu wengi na wale ambao maoni yao yanatiliwa maanani sana na umma wakati wa safari zangu Istanbul (Uturuki), Kairo (Misri), Khartoum (Sudan), Tashkeny na Samarqand 8Uzbekistan), New Delhi, Aligarh, Mumbai na Cochin (India), Jakarta na Jogjakarta (Indonesia), Abuja, Jos, Kano, Zaria (Nigeria9 baina ya Januari 2004 na Septemba 2006). Kutokana na masaada wa watafiti wa kienyeji, niliweza kufanya mahujiano, mijadala ya wazi na semina. Pia nilitoa mihadhara ya umma kwa wasilikizaji wa Kiislamu wakati wa matembezi ya sehemu zote hizo, ikiwa ni pamoja na mahali mbali mbali Ulaya na Amerika. Katika viwango mbali mbali vya harakati hii, nilifanyia marudio tena na kupanua karatasi ya kwanza ya mawazo yangu kutokana na maoni ya kichambuzi na mapendekezo niliyopata na kuendelezwa wakati wa harakati hizo.
Jambo lingine muhimu la harakati hii ya kusambaza ni kwamba muswada wa mda wa Kiiengereza ulitafsiriwa kwa Kiarabu, Bahasa Indonesia, Kibengali, Kifaransa, Kifarsi, Kirusi, Kituruki na Kiurdu. Miswada yote hii iliwekwa kwenye utandawazi wa anwani (www.law.emory.edu/fs) ambayo ilianzishwa kutoka Emory Law School ya Cho Kikuu cha Emory, huko Amerika mnamo July 2006 kwa madhumuni ya kuchochea mjadala katia lugha zao wenyew kuhusu mawazo ambayo yameelezwa kwenye utafiti huu. Wasomaji pia wanaweza kupata mswada katika lugha zao wenyewe na kuwasilisha majibu yoyote ambayo wangekuwa nayo katika lugha hiyo kupitia anwani ya barua pepezi maalumu ambayo inasimamiwa na mtafsiri ambaye ni msemaji wa lugha hiyo kama lugha yake ya mama. Kutilia mkazo huku kwa kufanya mswada huu na maingiliano yake kwenye matokeo yake katika lugha za kiasili za jamii za kiislamu inakuwa na umuhimu wa kitekelezi na kialama kwa madhumuni ya utafiti kwa ujumla. Lakini ukariri huu juu ya lugha za kienyeji kusichukuliwe kuwa kunapunguza thamani ya kufanya mswada huu upatikane kwa Kiiengereza ambayo inasomwa na Waislamu zaidi kote ulimwenguni kuliko lugha nyingine yoyote. Ni kweli kwamba wale ambao wanasoma kiiengereza aghlabu huwa ni wale watu wa tabaka la katikati na watu waliosomea makazi, lakini hao ni nishati kuu katika kuleta mabadilko katika jamii zote.
Katika harakati hii yote, nimebahatika kuweza kupata usaidizi na ushirikiano wa watu wengi sana na taasisi kuweza kuwatanbua wote hapa, lakini wanaofuata wanastahili kutajwa kimaalumu. Kwanza kabisa, nafurahi sana kutaja kwa shukurani kubwa msaada wa kifedha ambao ulitolewa na Wakfu wa Ford (Ford Foundation) na usaidizi wa kiufundi na kiusimamizi wa Markazi ya Utafiti wa Sheria na Dini wa Kitivo cha Sheria cha Emory (Center for the Study of Law and Religion Emory School of Law). Harakati yote ya utafiti na kazi ya kusambaza hazingewezekana bila ushirikiano wa kisomi na mchango wa Dkt. Rohit Chopra wa Chuo Kikuu cha Emory, ambaye pia alisimamia semina na mihadhara huko India. Kazi hii ilisimamiwa kule Indonesia na Chaider S. bamualim, Irfan Abubakar na Muhammad Jadul Maula; Uturuki na Recep Senturk na Somnur Vardar; na huko Uzbekistan na Aizada A. Khalimbetova. Pia shukrani zangu kwa watafiti wa kienyeji wegi na hasa Fazzur Rahman Siddiqe na V.A. Mohamed Ashrof kule India; Hisyam Zaini na Ruhaini Dzuhyatin kule Indonesia; Hani Ali Hassan na Mohamed Salah Abu Nar kule Misri; na Rasha Awad Abdallah kule Sudan.
........
Download Swahili